Wednesday 16 July 2014

Angellah Kairuki awaangukia watetezi wa haki za kisheria


NA MWANDISHI WETU
NAIBU Waziri wa Katiba na Sheria, Angellah Kairuki, amewaomba watetezi wa haki za kisheria, kuisaidia jamii ili kuondokana na changamoto ya kusuasua mahakamani kwa kesi za ukatili wa kjinsia, ardhi, ndoa na mirathi.
Amesema kitendo cha kusua sua kwa kesi hizo, kimekuwa kikimuumiza kichwa, hivyo wadau hao ni muhimu  ili kuwa na jamii salama.
Hayo aliyasema mjini Dar es Salaam, jana, wakati wa ziara yake ya siku tano ya kutembelea asasi zinazotoa misaada wa kisheria.
“Kutokana na kusuasua kwa kesi nyingi za ardhi, ndoa na mirathi mahakamani, watendaji wa haki za kisheria ni watu muhimu katika kuokoa jahazi.
“Wanatakiwa kuhakikisha  wanaisaidia jamii katika kutoa elimu na msaada zaidi wa kisheria ili kuwezesha upatikanaji wa haki kwa jamii ya wengi waliokata tamaa,” alisisitiza.
Kwa mujibu wa waziri huyo, jamii kubwa imekata tamaa ya kupata haki kutokana na ucheleweshwaji wa  kesi nyingi mahakamani, hususan zinazoigusa jamii zikiwemo za ardhi, ndoa na mirathi ambazo zimekuwa zikikwamisga harakati za maendeleo.

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru