Wednesday, 16 July 2014

Ndikilo: Sina mpango wa jimbo


NA BLANDINA ARISTIDES MWANZA
MKUU wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Evarist Ndikilo, amesema hana ndoto ya kugombea ubunge katika jimbo la Nyamagana kama inavyodaiwa.
Mhandisi Ndikilo alitoa kauli hiyo jana, baada ya mbunge wa jimbo hilo, Ezekia Wenje, kudai kuwa mkuu huyo wa mkoa anataka kugombea jimbo hilo.
Wenje alitoa tuhuma hizo mwishoni mwa wiki, kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa shule ya msingi Tambuka Reli, jijini hapa.
Katika mkutano huo, Wenje alitumia muda mwingi kutoa lugha za kejeli na kuwakashifu viongozi wa serikali, akiwemo Mhandisi Ndikilo na Meya wa Jiji la Mwanza, Stanislaus Mabula.
Wenje alidai Mabula ni meya wa kichina na hafai kuwaongoza madiwani wa jiji hilo na kwamba, mkuu wa mkoa huo, anataka kugombea ubunge wa Nyamagana wakati hana uwezo wa kuongoza.
Hata hivyo, Mhandisi Ndikilo alisema hana mpango wa kugombea ubunge kama Wenje anavyodai.
√¨Hayo madai yake hayana ukweli wowote, nadhani ameanza kupata wasiwasi, nimeteuliwa na Rais kuongoza mkoa wa Mwanza, wenye takribani watu milioni mbili, siwezi nikawaacha nikagombea ubunge,” alisema.

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru