Saturday, 12 July 2014

Atumia kamba za viatu kujiua


NA JESSICA KILEO
WATU wawili wamefariki dunia mjini Dar es Salaam katika matukio mawili tofauti, likiwemo la Godfrey Mtenga kukutwa akiwa amejinyonga hadi kufa.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Camilius Wambura, alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 4.00 asubuhi katika eneo la Kibangu Makoka, ambapo Mtenga alikutwa akiwa ananing’inia baada ya kujinyonga kwa kutumia kamba za viatu alizozitundika juu ya tawi la mti.
Wambura alisema, walikuta mwili wa mtu huyo ukiwa unaning’inia huku chini yake kukiwa na chupa mbili za pombea aina safari, viroba na kasha la sigara aina ya Embassy na kwamba, inaaminika alitumia vileo hivyo kabla ya kujininginiza.
Alisema, kwa mujibu wa taarifa zilizotoka kwa ndugu wa karibu wa mtu huyo, Seth Nassib, alimpigia simu siku chache kabla ya kifo chake na kumuomba amtunzie familia yake ambayo iko mkoani Kilimanjaro.
Kamanda alisema, ndugu huyo alipomuuliza kwa nini alisema hivyo hakuwa na jibu hadi alipopata taarifa ya kifo chake. Maiti yake imehifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala.
Katika tukio lingine lililotokea eneo la makutano ya barabara ya Bibi Titi Mohamed, mwanaume asiyefahamika anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 25 hadi 30 aligongwa na gari na kufariki dunia papo hapo.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi, alisema tukio hilo lilitokea juzi asubuhi saa 5.30, ambapo gari ambalo halikufahamika namba za usajili wala dereva, aina ya Toyota Land Cruiser likitokea eneo la Baridi kwenda barabara ya Morogoro lilimgonga mtu huyo aliyekuwa akitembea kwa miguu.
Marietha alisema mtu huyo alikuwa akivuka barabara akitokea mtaa wa Mkunguni kwenda Soko la Kisutu na kwamba, alifariki dunia mara tu alipogongwa na dereva kutokomea kusikojulikana. Mwili wa mtu huyo umehifadhiwa katika Hospitali ya Amana na upelelezi 

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru