Saturday 12 July 2014

Ashauri adhabu ya kifo ifutwe


Clarence Chilumba, Mtwara
Serikali imeshauriwa kutafuta njia mbadala kwa watuhumiwa wanaohukumiwa adhabu ya kifo na badala yake wapewe adhabu nyingine ambayo itawapa nafasi ya kuendelea kuzalisha mali.
Ushauri huo umetolewa na Mkurugenzi wa Utetezi na Maboresho wa Kituo cha Haki za Binadamu (LHRC), Arnold Sungusia,  wakati akiwasilisha mada juu ya haki za binadamu kwenye mkutano mkuu wa jukwaa la wahariri.
Alisema ni vyema serikali ikaweka sheria na adhabu mbadala kwa watu wanaohukumiwa adhabu ya kifo ili waweze kuendelea na shughuli za uzalishaji mali kwa lengo la kuwasaidia wengine.
Sungusia alisema kwamba, mtuhumiwa wa mauaji anapopewa adhabu ya kifo haimsaidii kujirudi kwani anaponyongwa serikali inakuwa imepoteza nguvu kazi ambayo ingeweza kuzalisha kipato ambacho kingeweza kuwasaidia watu wengine.
ìNi vyema kuwe na adhabu mbadala kwa wale wote wanaohukumiwa adhabu ya kunyongwa na kwamba, serikali ingewatengenezea gereza maalumu ambalo wangekuwa wakifanya shughuli za uzalishaji ikiwa ni pamoja na kuanzishwa kwa mfuko maalumu wa watu hao, ili kipato kinachotokana na shughuli zao kiweze kuwasaidia wanaobaki kama wajane, watoto na yatima,î alisema Sungusia

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru