Sunday, 13 July 2014

BREAKING NEWS!!! - KAFULILA KUPANDISHWA KIZIMBANIDavid Kafulila (Mbg)

SAKATA la Kampuni ya Kufua Umeme ya Independent Power Tanzania (IPTL), kutuhumiwa kuchota fedha katika akaunti ya Escrow, limechukua sura mpya baada ya kampuni hiyo kuamua kumburuta mahakamani Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR-Mageuzi) na kumfungulia kesi ya madai ya sh. bilioni 310.

IPTL kwa kushirikiana na Kampuni ya Pan African Power Solutions (T) Limited na Mtendaji Mkuu wa kampuni hizo, Harbinder Sign Seth, wamemburuta Kafulila katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam na kumfungulia kesi ya madai kutokana na kashfa anazodaiwa kuzitoa juu ya kuchotwa fedha katika akaunti ya Escow isivyo halali.
HABARI ZAIDI SOMA GAZETI LA UHURU KESHO!

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru