Wednesday, 9 July 2014

Mwenyekiti Chadema 'aichanachana' mkutanoni


NA CHARLES CHARLES, SONGEA
MWENYEKITI wa Chadema wa Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma, Mchungaji Desderius Haule, amesema chama hicho kinaendeshwa kibabe, kibinafsi na kama kampuni inayomilikiwa na watu wanaoweza kufanya chochote kwa jinsi wanavyotaka bila kufuata katiba.
Aidha, Haule amewashukia viongozi wa vyama vya upinzani kwa kueneza dhana potofu na uongo kuwa, kila mwanachama wao anayejiuzulu na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) anakuwa amenunuliwa.
Mchungaji huyo ambaye alikihama chama hicho na kurejea CCM kupitia mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Mwenyekiti wa Taifa wa Jumuia ya Wazazi,  Abdallah Bulembo kwenye Viwanja vya Sokoni mjini Mbinga, aliwataka wananchi kutoviamini vyama hivyo akisema havina malengo yoyote ya kuwasaidia.
Mimi nimerejea CCM kutokana na sababu mbalimbali ambazo ni pamoja na sera zake zinazotekelezeka, kuwa ndicho Chama pekee kinachoheshimu demokrasia na Chadema ni chama cha kibabe,Ă® alisema Mchungaji Haule alipokuwa akiwasalimia wananchi.
Katika salamu zake hizo wakati akitambulishwa na Bulembo kwenye Viwanja vya KibrangĂ­ombe vilivyopo katika Kata ya Lizaboni mjini hapa, alisema viongozi wa Chadema wamekuwa wakiongoza kwa ubabe na bila ya kufuata katiba ili kukidhi matakwa yao wenyewe.
Alitoa mfano kuwa, Septemba, mwaka jana, Mwenyekiti wa Chadema wa Mkoa wa Ruvuma, alikwenda Mbinga na kuitimua Kamati ya Utendaji ya Wilaya hiyo kwa tamko la mdomoni peke yake, hatua ambayo haiwezi kutokea ndani ya CCM.
Alisema kuwa hatua hiyo ilitokana na mmoja wa waliokuwa wagombea wa nafasi ya udiwani katika mojawapo wa kata zilizopo wilayani humo, kuwekewa pingamizi na aliyekuwa mgombea mwenzake wa nafasi hiyo wa CCM na kuondolewa katika mbio hizo.
Ajabu ni kuwa viongozi wa Chadema wenyewe wamekuwa mstari wa mbele kwa kuwawekea mapingamizi wagombea wa nafasi mbalimbali za dola wa CCM, lakini wao wakiwekewa inakuwa ni kosa linalopelekea viongozi wa ngazi za juu kwenda kuwatimua viongozi wa chini.
Kwa tabia hii ya Chadema, kama chama hicho kingekuwa madarakani basi hivi leo tungekuwa tunachimba mahandaki,alisema.
Akizungumza katika mkutano huo, Bulembo aliwaomba wananchi wasipotoshwe na madai ya genge linalojiita Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) akisema limepanga kuhujumu mchakato mzima wa kupata katiba mpya.

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru