NA THEODOS MGOMBA, DODOMA
WAKUU wa Idara za Raslimali watu katika Mamlaka za Serikali za Mitaa, wametakiwa kuhakikisha watumishi wanaoajiriwa kwa mara ya kwanza katika halmashauri zao, wanapewa mafunzo elekezi ndani ya miezi sita tangu kuajiriwa kwao.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Rehema Nchimbi, alitoa wito huo jana, wakati akifungua Mkutano wa Mwaka wa wakuu wa Idara za Utawala na Rasilimali Watu katika Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Alifungua mkutano huo kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani.
Dk. Rehema alisema mafunzo hayo ni muhimu kwa kuwa huwawezesha watumishi wapya kuuelewa utumishi wa umma na kufahamu misingi yake, sheria, kanuni na utaratibu wa utendaji kazi.
Alisema mtumishi akipata mafunzo atajua majukumu na wajibu wake kwa kuzingatia maadili na uadilifu kazini.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, George Yambesi, alisema menejimenti ya rasilimali watu katika mamlaka za serikali za mitaa ina changamoto nyingi ambazo zinahitaji msukumo wa pamoja katika kuzifanyia kazi.
Alisema mikutano kama hiyo inatoa fursa ya kujadili changamoto hizo, ambapo mada 11 zitawasilishwa na kujadiliwa na wajumbe kujadili.
Wednesday, 2 July 2014
Toeni semina elekezi kwa waajiriwa wapya- Dk. Nchimbi
08:29
No comments
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Toa Maoni Yako Kwa Uhuru