Wednesday 2 July 2014

Sheikh alia na wanaopaisha bei mwezi wa Ramadhani


NA SOLOMON MWANSELE, MBEYA
WAFANYABIASHARA wameaswa kutotumia mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhan, kujinufaisha binafsi kwa kupandisha bei za vyakula sokoni.
Baadhi ya wafanyabiashara wanatuhumiwa kuugeuza mwezi wa Ramadhan kuwa, ndio wa kuchuma zaidi kibiashara kwa kupandisha bei za bidhaa, zikiwemo viazi utamu, mihogo, maharage, magimbi na tambi ambavyo hutumiwa na wengi.
Katibu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Mkoa wa Mbeya, Juma Killa, alitoa angalizo hilo jana wakati akizungumza kuhusu hali ya chakula katika mwezi huu.
Killa alisema ikiwa ni chungu nne tangu mfungo huo uanze, tayari bei za viazi, mihogo, magimbi, tambi na maharage zimepandishwa katika masoko ya Matola, Uyole, Mbalizi, Mwanjelwa na Soweto, ambayo yamekuwa yanatumiwa zaidi na Waislamu kupata mahitaji yao.
“Hivi sasa bei za biadhaa hizi katika masoko hayo, zimepanda kwani fungu moja la viazi lililokuwa likiuzwa kwa sh. 500, sasa bei imepaa, linauzwa sh. 1,000, huku  magimbi yaliyokuwa yanauzwa sh. 1,000 sasa yanauzwa sh. 2,000,” alisema Killa.

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru