NA MWANDISHI WETU
RAIS Jakaya Kikwete amesifu uhusiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Afrika Kusini na kwamba haujawahi kuwa mzuri kama ilivyo sasa.
Amesema ni muhimu kwa Afrika Kusini kuendelea kuonyesha uongozi mzuri katika Ukanda wa Kusini mwa Afrika kwa sababu kwa kufanya hivyo,Afrika Kusini itakuwa inatimiza jukumu lake la kihistoria.
Rais Kikwete aliyasema hayo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki wakati akiagana na Balozi wa Afrika Kusini hapa Tanzania , Thanduyise Henry Chiliza aliyemaliza muda wake.
Alimwambia balozi huyo kuwa ni nchi chache duniani kwa sasa ambazo zina uhusiano wa karibu zaidi na Tanzania kama ilivyo kwa Afrika Kusini.
Hata hivyo, alibainisha kuwa uongozi wa Afrika Kusini katika eneo la Afrika ni jukumu la kihistoria la nchi hiyo ambalo ni lazima iendelee kulitimiza kwa kiwango kinachotarajiwa.
Naye Balozi Chiliza alisema anamshukuru Rais Kikwete kwa kumuunga mkono wakati wa uwakilishi wake na hivyo kumsaidia kutimiza majukumu yake ya kibalozi hapa nchini.
Wednesday, 2 July 2014
JK asifu ushirikiano TZ na Afrika Kusini
08:31
No comments
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Toa Maoni Yako Kwa Uhuru