Wednesday 11 March 2015

Ataka madaktari wa figo waongezeke


NA SYLVIA SEBASTIAN
SERIKALI imeombwa kutoa kipaumbele kwa wataalamu wanaotaka kusomea fani ya ugonjwa wa figo ili idadi ya madaktari bingwa iweze kuongezeka  katika  mikoa yote ya Tanzania.
Pia imeombwa kuangalia uwezekano wa kuwa na wawekezaji watakaotengeneza vifaa tiba vinavyohusiana na ugongwa wa figo na kuanzisha huduma ya upandikizaji wa figo hapa nchini.
Daktari  Bingwa wa Figo na Magonjwa ya Watoto katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Jacqueline Shoo, alitoa wito huo juzi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.
‘’ Tunapofikia kilele cha maadhimisho ya siku ya figo, tungependa kuiomba serikali yetu  kutoa kipaumbele kwa ugonjwa huu kwa kutenga fungu maalumu kwa ajili ya kuwahudumia wagonjwa wa figo,’’alisema.

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru