NA RACHEL KYALA
TUME ya Uchunguzi wa Operesheni
Tokomeza, inatarajia kuwasilisha taarifa yake kwa Rais Jakaya Kikwete, wakati
wowote kuanzia sasa.
Mwenyekiti wa Tume hiyo,
Jaji (mstaafu) Hamisi Msumi, alisema hayo alipozungumza na Uhuru jana na
kueleza kwamba wameshakamilika kazi.
Alisema walifanya
majumuisho ya taarifa na kukamilisha ripoti ambayo wanapaswa kumkabidhi Rais Kikwete.
“Wakati wowote kuanzia leo, tutamwomba Rais Kikwete atupangie siku ya kukutana naye ili tumkabidhi ripoti hiyo. Kwa kuwa yeye ndiye mwenye shughuli nyingi, atatupangia nafasi na sisi tuko tayari,” alisema.
Tume hiyo iliundwa na Rais
Kikwete, Mei mwaka jana, ili kuchunguza, kukusanya na kupokea taarifa juu ya malalamiko
juu ya mwenendo wa utekelezaji wa
Operesheni Tokomeza Ujangili nchini, hususan katika mikoa ya Arusha,
Manyara, Tabora, Singida na Dodoma.
Hatua ya Rais Kikwete ya
kuunda tume hiyo ilitokana na baada ya operesheni hiyo iliyoanza Oktoba 2013, kusitishwa
na Bunge Novemba 4, 2013, kutokana ukiukwaji wa sheria na haki za binadamu
wakati wa utekelezaji wake.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Toa Maoni Yako Kwa Uhuru