Tuesday, 3 March 2015

Ngeleja mbele ya Baraza la Maadili ya Watumishi wa Umma...

MBUNGE  wa  Sengerema ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, akiingia katika ukumbi wa Kariamjee, Dar es Salaam jana kuhojiwa na Baraza la  Maadili ya Watumishi wa umma kuhusiana na tuhuma za kukiuka sheria ya maadili katika sakata la akaunti ya Tegeta Escrow.

Ngeleja akisikiliza kwa makini  hoja  zilizokuwa zikitolewa na wanasheria wa Serikali(hawako pichani)  huku akiwa ameshika tama wakati kikao cha baraza hilo kikiendelea.

Ngeleja akikagua baadhi ya  nyalaka zake kwaajili ya kuwasilisha mbele ya baraza hilo ili vitumike kama ushahidi

William Ngeleja akijitetea mbele ya Baraza la maadili ya watumishi wa umma

Ngeleja akienda mbele ya baraza hilo kutoa ushahidi wake.

Ngeleja (kushoto) akiapishwa na mtumishi wa baraza hilo kabla ya kuanza kutoa ushahidi wake.Mkurugenzi wa Sheria  wa Wizara ya  Ardhi,  nyumba na  Maendeleo ya Makazi, Rugonzibwa  Mujunangoma akiwa mbele  ya Baraza hilo jana  akikabilia na thuma za kukiuka sheria ya maadili ya watumishi wa umma katika sakata la kuchota fedha katika akaunti ya Tegeta Escrow.

Mtu mwenye ulemavu akimpa pole Ngereja baada ya kuhojiwa.

Ngeleja akitoka nje ya ukumbi wa Kariamjee mara baada ya kuhojiwa.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru