Wednesday, 11 March 2015

Lukuvi awapa darasa maofisa ardhi


NA DOTTO MADUHU, MWANZA
WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wiliam Lukuvi, amewaagiza maofisa ardhi na wazee wa mabaraza ya ardhi, kuhakikisha wanatenda haki ya kutoa hukumu kwa wakati kuhusu mashauri ya ardhi.


Lukuvi alisema hayo jana katika ziara yake ya siku mbili mkoani hapa, na kuongeza kuwa lengo la ziara hiyo ni kutokana na kuwepo kwa malalamiko mengi kutoka kwa wananchi wa kanda ya ziwa.
Aliwaasa maofisa ardhi kuhudumia wananchi kwa haki na uzalendo bila kujali uwezo wao wa kifedha.
“Mnatakiwa kuhudumia wananchi wetu bila kujali itikadi zao, kifedha na hata kabila kwani wote ni wananchi wetu kwa kuwa tupo katika nchi moja,” alisema.

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru