Saturday, 14 March 2015

Dhambi ya ubaguzi inaiua CHADEMA


CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema dhambi ya ubaguzi ndani ya CHADEMA inaiua na sio kwamba kuna mkono wa CCM.
Kauli hiyo ilitolewa juzi na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, alisema hayo alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika katika mji wa Mto wa Mbu.
Nape alisema CHADEMA inaelekea kufa kutokana na kukumbatia dhambi ya ubaguzi na umwagaji wa damu za wananchi wasio na hatia.
ìTulijua watasema kuwa sisi CCM tumeingiza mkono wetu ndani ya chama chao, hiyo si kweli. Ukweli ni kuwa, chama hicho lazima kife kutokana na mfumo walionao,îalisema.

Alisema kutokana na chama hicho kujenga tabia ya kubagua watu hakitakuwa salama na ni lazima kitakufa.
ìHamuwezi kujenga chama huku mkiwa na ubaguzi ndani yake au kumwaga damu za watu, kila mnapokwenda kufanya operesheni ni lazima mmwage damu, hii haitamwagika bure,îalisema.
Nape alizitaja baadhi ya operesheni zilizofanywa na chama hicho na kugharimu maisha ya watu kuwa za Arusha, Morogoro, Iringa na Singida.
Alisema huko kote kimekuwa kikiendesha maandamano na kusababisha mauaji ya watu wasio na hatia.

Kwa mujibu wa Nape, hivi sasa hali ya chama hicho ni mbaya kutokana na kuwafukuza baadhi ya wanachama wake wakongwe kila kukicha akiwemo Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe.
ìHivi sasa vyama hivi vipo katika wodi ya wagonjwa mahututi na vinapumulia mashine na mwaka huu tutahakikisha tunatoa mashine hizo na kuviua kabisa kwa kushinda kwa kishindo katika uchaguzi mkuu ujao,îalisema.
Alisema hali ya kufukuzwa kwa Zitto si tukio la kwanza kwa kuwa wapo wengine wengi walishafukuzwa katika chama hicho kwa dhana ya ubaguzi.
Kwa mujibu wa Nape, wale waliofukuzwa katika chama hicho ni watu kutoka nje ya mikoa ya Kaskazini.
ìZitto si wa kwanza, wapo kina (Walid) Kaborou ambaye walikaa naye kisha wakamfukuza na wengine kama Chacha Wangwe ambaye baada ya kuhoji mambo mbalimbali kilichomtokea wote tunajua,îalisema.
Nape alisema hali hiyo ya ubaguzi ndiyo chanzo cha kufa kwa chama hicho kwa kuwa ni ha kikanda na si kwa maslahi ya Watanzania wote.
Aliwaasa vijana wa Mkoa wa Arusha kuachana na chama hicho chenye ubaguzi kwa kuwa wakati wake wa kufa umefika.

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru