NA REHEMA MAIGALA
WAZIRI wa Viwanda na Biashara,
Dk. Abdallah Kigoda amewataka wajasiriamali wanaoanza biashara zao wasiwe
wanalipishwa kodi mpaka baada ya miaka mitatu.
Amesema kuwalipisha
kodi wajasiriamali hao kunasababisha biashara zao kutoendelea na kutofikia
malengo waliyojiwekea katika uendelevu wa biashara na maendeleo kwa jumla.
Akizungumza na Uhuru jana jijini Dar es Salaam, Dk. Kigoda alisema
kuwalipisha kodi wajasiriamali ambao ndio kwanza wanaanza, kunawaharibia
malengo yao.
“Tuige mfumo wa nchi ya Malaysia ambao mjasiriamali akianza biashara yake hatakiwi kulipishwa kodi mpaka baada ya miaka mitatu.
Alisema suala la wajasiriamali kutolipa kodi
atalipeleka mbele ya bunge ili liweze kujulikana kwa uwazi.
Dk. Kigoda alisema wanatarajia
kuanzisha viwanda mama ili vijana waweze kupata ajira za kudumu na kwamba viwanda
hivyo vitakaa kwa muda mrefu kwa kuwa vitakuwa na bidhaa za kudumu.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Toa Maoni Yako Kwa Uhuru