Tuesday, 3 March 2015

SHUGHULI YA KUUAGA MWILI WA KAPT. KOMBA, VIWANJA VYA KARIAMJEE


RAIS Jakaya Kikwete na mkewe Mama Salma, wakitoa salamu zao za mwisho.

RAIS Dk. Jakaya Kikwete akimfariji mke wa marehemu, nyuma yake ni wanafamilia.

SPIKA wa Bunge, Anne Makinda, akitoa heshima za mwisho.

MKE wa Marehemu akiuaga mwili

KATIBU wa Siasa na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi akitoa heshima za mwisho

KATIBU Mkuu wa CCM, Abrahman Kinana, akipiga saluti ya heshimu kwa mwili wa Kapt. Komba

KAMISHNA wa Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alikuwepo

Miongoni mwa waombolezaji, alikuwepo Katibu Mkuu wa Chama cha CHADEMA, Dk. Wilbrod Slaa

RAIS Mstaafu, Benjamin Mkapa (kushoto), akibadilishana mawazo na Katibu Mkuu wa CCM.

JENEZA lililohifadhiwa mwili wa marehemu Kapt. John Komba likiwa limebebwa na Maofisa wa Bunge.

KIKUNDI maalum cha wimbo wa maombolezo kikiimba katika msiba huo.

Baadhi ya waombolezaji

WAOMBOLEZAJI wakiwa kwenye mstari wa kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Kapt. John Komba

MWAKILISHI wa Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Joshua Nassari akitoa salamu kwa familia na waombolezaji waliofika kwenye shughuli hiyo.

MARAIS wastaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Benjamin Mkapa (kushoto) na Ali Hassan Mwinyi wakisalimiana mara baada ya kumalizika kwa shughuli hiyo. 

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru