Saturday, 14 March 2015

CCM kuvalia njuga utalii


Kinana amesema Chama kitahakikisha sekta ya utalii inakua kadri ilivyopangwa.
Pia amesema nchi imepiga hatua, lakini bado kuna tatizo la urasimu katika maeneo mengi.
Katibu Mkuu alisema hayo alipozungumza na wakazi wa mji wa Mto wa Mbu mkoani Arusha.
Alisema urasimu ndani ya sekta mbalimbali ikiwemo ya utalii umekuwa kikwazo kwa wawekezaji.
ìMtu anakuja leo unamwambia aje kesho na kila siku jambo hilo linajirudia ndiyo chanzo cha watu kukata tama,îalisema.
Alisema CCM ni Chama chenye dhamana na ndicho kilicho na Ilani na kuisimamia serikali, hivyo kitakuwa kikali katika kuhakikisha sekta hiyo inakua.
ìYapo maeneo ambayo serikali inafanya vizuri na ni wajibu wetu kuisifia, lakini kwa yale ambayo hawafanyi vizuri hatuna budi kuisema na kuikemea,îalisema.
Kinana alisema CCM ni Chama pekee chenye serikali na ndicho kinachoweza kutekeleza mambo mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi.
Alisema vyama vingine pamoja na kujifanya kuwa na Ilani zao, hawana serikali hivyo hawawezi kutekeleza jambo lolote.

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru