Tuesday 17 March 2015

Muswada wa taasisi za kifedha waja


NAIBU Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, amesema serikali itapeleka bungeni  muswada wa sheria ambao utawawezesha wananchi kuanzisha taasisi za kifedha.

Mwigulu alisema hayo jana bungeni mjini Dodoma wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Igunga, Dk. Dalaly Kafumu, aliyetaka kujua lini serikali itawawezesha wakazi wa Igunga kuanzisha  taasisi za kifedha.
Mwigulu alisema muswada huo utaandaliwa na kupelekwa bungeni wakati wowote kuanzia sasa.
Katika swali la msingi, Dk. Kafumu alitaka kufahamu ni lini serikali itaongeza benki nyingine kwa wananchi wa Wilaya ya Igunga.
“Serikali imeweka sheria na utaratibu kusaidia nguvu na juhudi za wananchi kuanzisha benki au taasisi za kifedha katika maeneo yao zikiwemo benki za kijamii na taasisi ndogo za kifedha,” alisema
Kuhusu kuwawezesha wananchi wa Igunga kuanzisha huduma za kifedha na taaisisi za fedha, alisema tayari wameshafanya mazungumzo na Benki ya CRDB na muda mfupi huduma hizo zitapelekwa.

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru